Translate

Wednesday, May 18, 2016

ANGALIA MABIGWA WA LIGI KUU TANZANIA BARA WAKABIDHIWA KOMBE.



Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea kwa Bingwa wa Ligi Kuu klabu ya Dar es Salaam Young Africans kucheza mchezo wake wa 29 dhidi ya Ndanda FC uwanja wa
Taifa Dar es Salaam, licha ya kuwa Yanga tumezoea kumuona Taifa kama mwenyeji ila leo yeye ndio alikuwa mgeni wa Ndanda FC ambao walikubali kuchezea Taifa kama uwanja wa nyumbani.








Katika mchezo huo wa kukamilisha ratiba ya Ligi Kuu klabu ya Dar es Salaam Young Africans ambao ndio Mabingwa wa Ligi Kuu kwa kutetea taji hilo mara mbili mfululizo, wamelazimishwa sare ya goli 2-2, Ndanda FC ndio walianza kufunga goli kwa mkwaju wa penati dakika ya 28 kupitia kwa Omary Mponda.


Kamusoko, Ngoma wakiwa na wake zao pamoja na nahodha wao Cannavaro.


Haruna Ninyonzima akiwa na mkewe pamoja na watoto wake mapacha

Yanga walifanikiwa kusawazisha goli dakika ya 36 kupitia kwa Simon Msuva, lakini dakika ya 40 Donald Ngoma akapachika goli la pili kwa Yanga na kuwafanya Yanga kuwa mbele kwa goli 2-1, Yanga waliendelea kuutawala mchezo katika uwanja ambao umejaa mashabiki wake ambao wanasubiria kuona Kombe likabidhiwa,  kujisahau kwa Yanga kuliwafanya Ndanda FC kuchomoa goli dakika ya 80 kupitia kwa Atupele Green

Ngoma ambaye leo ndio ametwaa taji lake la kwanza akiwa na mkewe.


Nonga na Yondani baada ya mechi kumalizika.

Kutoka kushoto Jery Muro, Ngoma na mkewe wa Ngoma.

kutoka kushoto Jery Muro, Ngoma na mke wa Ngoma. 

Haruna Niyonzima na mtoto wake.

kamusoko akiwa na mtoto wake tshani na mkewe

kamusoko akiwa na familia yake na bendera ya nchi yake Zimbabwe.

ngoma na mkewe.











No comments: