Translate

Thursday, June 23, 2016

MUHIMBILI KUMALIZA TATIZO LA UCHANGANYAJI MAITI.



Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru ametengua uteuzi wa mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi Dkt Praxeda Ogweyo kuanzia leo June 23, 2016 ili kupisha uchunguzi kutokana na kushindwa kusimamia vizuri maiti wakati wa
kuzitoa kwa ndugu mara mbili katika kipindi kisichozidi miezi mitatu na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wafiwa na Hospitali kwa ujumla.

Prof. Museru amemteua Dkt.Flora Lwakatare Mkuu wa idara ya Radiolojia kukaimu nafasi hiyo.Kurugenzi ya Tiba Shirikishi inasimamia idara ya mionzi na idara ya Maabara ambapo kitengo cha kuhifadhi maiti kipo chini maabara.Vilevile Prof. Museru ametengua uteuzi wa Mkuu wa kitengo cha kuhifahi maiti Hospitali ya taifa Muhimbili Dkt. Innocent Mosha na kumteua Dkt Herbert Nguvumali kukaimu nafasi hiyo

                       

                          MUHIMBILI KUTOA MATIBABU YA MOYO BURE.


1 comment:

Unknown said...

बड़े नोट बंद होने से शेयर बाजारों में जबरदस्त गिरावट
Read more todaynews18.com https://goo.gl/GTqCZ9