pichani ni aliekua waziri wa mambo ya ndani ya nchi Charles Kitwanga.
Moja ya
habari iliyoripotiwa ni hii kutoka gazeti la Habari Leo yenye kichwa cha
habari
‘Kitwanga: Yaliyotokea namwachia Mungu, asema amerudi na nguvu mpya, kutua
bungeni wiki ijayo’
Gazeti la
Mtanzania limeripoti kuwa aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Charles
Kitwanga amesema yupo imara na amerejea nchini akiwa na matumaini mapya, pamoja
na hali hiyo, amesema kuwa hivi sasa anajipanga kufanya kazi usiku na mchana
kuhakikisha anasaidia nchi pamoja na wapiga kura wake na maendeleo ya kweli.
Kauli hizo
alizitoa Dar es salaam jana alipozungumza na Gazeti la Mtanzania katika
mahojiano maalumu baada ya kurejea akitokea nchini Israel ambako alikwenda kwa shughuli zke binafsi,
Gazeti hilo limemnukuu akizungumza haya………
>>>’niko
imara kabisa na nina nguvu na matumaini mapya, nimeingia nchini juzi nikitokea
nchini Israel ambako nilikuwa na shughuli zangu binafsi, unajua mimi ni mtaalamu
(wa mawasiliano) na wewe unajua kabla sijaingia kwenye siasa nilikuwa nafanya
nini’.
>>>’kifupi
nasema nilikwenda Israel kwa shughuli zangu binafsi kabisa ambazo kwa kipindi
cha wiki tatu nilizokuwa huko nimefanya. hata wanaosema nilikwenda kulia kwa Bwana
nao ni mawazo yao, maana unajua ile ni nchi takatifu kutokana na historia yake’
No comments:
Post a Comment