Translate

Thursday, June 23, 2016

SOMA ALICHOKISEMA ZITO KABWE BAADA YA KUTOKA POLISI.



Baada ya polisi kuzuia kongamano la Bajeti lililokuwa limeandaliwa na chama cha ACT-Wazalendo ambapo kongamano hilo lililenga kumpa fursa ya pekee kiongozi wa chama hicho Zitto Kabwe kusema yale ambayo angeyasema bungeni baada yeye na wabunge wenzake sita wa upinzani kusimamishwa kuhudhuria vikao vya bajeti bungeni.


Baada ya taarifa kuripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari kwamba kiongozi huyo wa chama alikuwa akitafutwa na polisi bila mafaniko leo June 13 2016 amejitokeza mbele ya wanahabari na kuzungumza hizi sentensi.

'Mpaka sasa polisi hawajatupa taarifa rasmi kwa nini wamezuia kongamano la bajeti'-Zitto Kabwe pic.twitter.com/7EdIeLXHHe

— mosktear blog (@mpyamjini.blogspot.com) June 13, 2016

'Polisi walitaka kunikamata kwa kunivizia ili nisiwepo kwenye kongamano lakini tukachukua hatua ili wasiweze'-Zitto pic.twitter.com/EzbxDXo6Mz

— mosktear blog (@mpyamjini.blogspot.com) June 13, 2016

'Hatufahamu ni nini watawala wanakificha ndani ya bajeti kwani makongamano, mikutano inazuiwa'-Zitto Kabwe pic.twitter.com/tieIbjFiiZ

— mosktear blog (@mpyamjini.blogspot.com) June 13, 2016

'CCM wakae na kiongozi wao wamwambie, wasiomuogope kwani anachokifanya Rais ndani ya nchi yetu sio sahihi'-Zitto Kabwe

— mosktear blog (@mpyamjini.blogspot.com) June 13, 2016

'sisi tumeamua tutaendelea na kongamano letu hapa ofisini kwetu tutawaalika watanzania tujadili bajeti'-Zitto kabwe

— mosktear blog (@mpyamjini.blogspot.com) June 13, 2016


'Polisi wananihitaji wafuate utaratibu, ofisi zetu zipo, simu zipo wasituvizie viongozi, wiki iliyopita walinipigia simu nilikwenda'-Zitto

No comments: