Translate

Tuesday, May 17, 2016

MAAMUZI YA CANNAVARO KAMA MKWASA ATAAMUA NYOTA HUYO AJIUNGE NA KIKOSI CHA TAIFA STARS.


          
              Baada ya headlines za muda mrefu kuhusu aliyekuwa nahodha wa timu ya taifa yaTanzania  Nadir Haroub Cannavaro kutangaza
kustaafu kuchezea timu ya taifa yaTanzania kutokana na kuvuliwa unahodha bila kupewa taarifa rasmi, tuliwahi kusikia kocha wa Taifa Stars Boniface Mkwasa akisema kuwa bado Cannavaro yupo katika mipango yake.

mpyamjini.blogsport.com ilimpata katika exclusive interview na kumuuliza vipi kama Mkwasa akimuita katika kikosi cha Taifa Stars kitakachocheza na Kenya May 29 “Kwanza ieleweke sina tatizo na kocha Mkwasa hata kidogo ni kocha ambaye napenda kufanya nae kaza akiniita nitamtafuta tutakaa chini kushauriana kiutu uzima halafu nitamwambia mimi naomba tu kwa sasa niendelee kupumzika kuchezea Stars”.


No comments: