Chama cha soka nchini Uingereza FA May 16
kimetangaza adhabu kwa
vilabu vya Chelsea na
Tottenham amabavyo vinatoka jiji moja la London, FA wametangaza
uamuzi wa kuvipiga faini vilabu hivyo kutokana na kushindwa kuwadhibiti
wachezaji wake kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu.
FA imetangaza kuipiga faini Chelsea ya pound 375,000
ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 1 ya kitanzania, wakati klabu ya Tottenham Hotspurs
imepigwa faini ya pound 225,000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 700 za
kitanzania, maamuzi yamefanyika kutokana na wachezaji wa timu hizo kufanyiana
vitendo visivyo vya kinidhamu wakati wa mchezo dhidi yao.
Mechi hiyo ambayo ilichezwa Stamford
Bridge ilimalizika kwa sare
ya goli 2-2, lakini muamuzi alitoa jumla ya kadi za
njano 12,
hata hivyo mapema mwezi huu Dembele wa
Tottenham alifungiwa
mechi sita kutokana na kumpelekea vidole Diego
Costa wa Chelsea
machoni kwa makusudi.
No comments:
Post a Comment