Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru
ametengua uteuzi wa mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi Dkt Praxeda Ogweyo
kuanzia leo June 23, 2016 ili kupisha uchunguzi kutokana na kushindwa kusimamia
vizuri maiti wakati wa
kuzitoa kwa ndugu mara mbili katika kipindi kisichozidi
miezi mitatu na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wafiwa na Hospitali kwa ujumla.
Prof. Museru
amemteua Dkt.Flora Lwakatare Mkuu wa idara ya Radiolojia kukaimu nafasi
hiyo.Kurugenzi ya Tiba Shirikishi inasimamia idara ya mionzi na idara ya
Maabara ambapo kitengo cha kuhifadhi maiti kipo chini maabara.Vilevile Prof.
Museru ametengua uteuzi wa Mkuu wa kitengo cha kuhifahi maiti Hospitali ya
taifa Muhimbili Dkt. Innocent Mosha na kumteua Dkt Herbert Nguvumali kukaimu
nafasi hiyo
1 comment:
बड़े नोट बंद होने से शेयर बाजारों में जबरदस्त गिरावट
Read more todaynews18.com https://goo.gl/GTqCZ9
Post a Comment